Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kuangamia kwa kamanda mashuhuri wa kikundi hicho cha kigaidi zimesambazwa na kuthibitishwa katika vyombo vya habari nchini humo
Zahrani Alwash ambaye ndiye kamanda mkuu wa kikundi cha kigaidi cha Jaishul Islamu ameuwawa katika shambulio la anga liliofanywa na majeshi ya Urusi katika kikao walichokuwa wakifanya magaidi hao katika mji wa Utaya sehemu ya (Ghutatul Sharshqiya) katika wilaya ya Humeh mkoani Damascuas.
Majeshi ya Urusi yalikuwa yakifuatilia kwa makini kikao hicho cha magaidi hao hatimaye Ndege moja ya kivita ya Urusi kufanya shambulio la anga katika sehemu hiyo ya kikao hicho cha makamanda wa kikundi hicho na kusababisha kuangamia kwao.
Zahrani Alwash miaka mine iliopita aliasisi kikundi cha kigaidi kilichokuwa na jina la (Liwaul Islam) katika wilaya Humeh Damascus ambapo kikundi hicho baada ya miaka kadhaa kupita kilibadirika na kilipata nguvu kubwa katika wilaya hiyo hatimaye kubadirishwa jina lake na kuitwa (Jaishul Islamu).
Baadhi ya nchi kubwa za kiarabu ziliunga mkono harakati za kigaidid za kikundi hicho na kukipa nguvu za kimali na vifaa vya kivita ambapo kamanda huyo mara kwa mara alikuwa akisafiri kwenda katika nchi hizo ikiwemo nchi ya Saudi Arabia.
mwisho wa viongozi/290